Jeremiah 8:10-12


10 aKwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,
na mashamba yao kwa wamiliki wengine.
Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,
wote wana tamaa ya kupata zaidi;
manabii na makuhani wanafanana,
wote wanafanya udanganyifu.

11 bWanafunga majeraha ya watu wangu
bila uangalifu.
Wanasema, “Amani, amani,”
wakati hakuna amani.

12 cJe, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno?
Hapana, hawana aibu hata kidogo,
hawajui hata kuona haya.
Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,
watashushwa chini watakapoadhibiwa,
asema Bwana.

Copyright information for SwhKC